Kufuatia tukio hilo, Taifa la Botswana limelifunga kanisa la muhibiri huyo wa Malawi mwenye utata anayedaiwa ''kutembea angani''.
Serikali ilithibitisha kufungwa kwa kanisa la Bushiri la Christian Gathering Church ECG mjini Gaborone mara kadhaa kutokana na wasiwasi kuhusu ''fedha za miujiza''.
Chombo cha habari cha Malawi24 kimeripoti kwamba kanisa hilo lilipinga uamuzi huo mahakamani uliochukuliwa chini ya mwaka mmoja baada ya muhibiri huyo kupigwa marufuku kuingia nchini humo.
Alikuwa ametarajiwa kuhudhuria kongamano fulani.
Hatahivyo waziri wa Botswana Edwin Batshu alitangaza mnamo mwezi Aprili 2017 kwamba bwana Bashir ambaye sasa anaishi Afrika Kusini atahitaji Visa ili kuingia, licha ya raia wa Malawi kutohitaji kibali hicho kulingana na chombo cha habari cha AllAfrica.com
Gazeti hilo limeongezea kwamba ni hatua ya kanisa hilo kutumia ''fedha za miujiza'' ambayo imevunja sheria za taifa hilo.
Bwana Bushiri ambaye ana zaidi ya ''likes'' milioni 2.3 katika mtandao wa facebook na ambaye alivutia umati mkubwa wa kuweza kujaza uwanja wa FNB mkesha wa mwaka mpya bado hajatoa tamko lolote.
Kanisa hilo ni maarufu kwa mtindo wake wa maisha ya kifahari kutokana na ufanisi wake ambao umevutia wafuasi wengi barani Afrika.
Alishutumiwa mwaka uliopita baada ya kubainika alikuwa akiwatoza kati ya dola 80 hadi 2000 wafuasi wake waliotaka kuhudhuria chakula cha jioni naye kulingana na chombo cha habari cha Afrika Kusini South Africa News24
TOA MAON YAKO HAPA!
No comments:
Post a Comment