Lugha ya alama nini?
Lugha ya alama Tanzania ni chombo cha mawasiliano ambacho humuwezesha mzungumzaji kufikisha ujumbe kwa jamii kwa hadhira iliyokusudiwa na jamii husika.
Lugha ya alama imegawanyika katika makundi mawili;
1. Alama kwa njia ya herufi (alphabet)
2. Alama kwa njia ya ishara.
Katika mada hii ntaongelea zaidi kipengele cha kwanza ambacho ni ALAMA KWA NJIA YA HERUFI..
Kwanini?
Kwa sababu kipengele hiki ni rahisi kumfundisha mtu aliye mbali na akaelewa mfano hapa JAMII FORUMS.
Kipengele cha pili hufundishwa MUBASHARA .
Tulisongeshe,
ALAMA KWA NJIA YA HERUFI (ALPHABET)
Herufi A, B, C,D,E,F,G, H,I,J, K, L, M,N,O mpaka Z huweza kuandikika kwa kutumia vidole vyetu.
Mbinu gani hutumika?
Mbinu zitumikazo hapa ni kukunja vidole kwa kufuata umbo la herufi husika.
Mfano herufi "C" ukitizama katika picha hapo chini utaona KIDOLE GUMBA na vidole vingine vimekunjwa kuunda shape ya herufi C. Utaratibu huu pia hutumika katika kuandika herufi zinazo fuata.
NB: Herufi "I" na "J" katika picha utaona kama zinafanana, utaratibu wa kuzitofautisha upo hivi, UKITAKA KUANDIKA HERUFI J ANZA KWA KUANDIKA HERUFI ,"I" THEN KUWA KAMA UNACHORA HERUFI J HEWANI.
Wakuu TUMIENI umakini kuchunguza MIKUNJO YA VIDOLE pamoja na alama husika mtagundua mikunjo ya vidole na imekunjwa kwa kufuata UMBO LA HERUFI HUSIKA. Mfano mzuri tizameni herufi Y.
HERUFI HIZI HUTUMIKA JE?
Herufi hizi hutumika kwa kuandika neno au maneno uliyokusudia kwa mhusika (kiziwi) kwa kufuata herufi tajwa hapo juu katika picha.
Jaribu sasa kwa kuanza na maneno kama DADA, KAKA, MAMA, BIBI n.k,
Ni rahisi sana na utaweza kuwasiliana au kuongea na kiziwi yeyote.
Karibuni kwa nyongeza , maoni, hoja na maswali.
Ahsanteni.
SOURCE: JamiiForums
LUCKDUBEJF-Expert Member
No comments:
Post a Comment