SUBSCRIBE TO OUR YOUTUBE CHANNEL-Shec Media.........LIKE OUR FACEBOOK PAGE-Shec Media..... FOLLOW US ON INSTAGRAM-@shecmedia_tz........WHATSAPP NUMBER +255 752 0133 43

Tuesday, December 19, 2017

MAULID MTULIA Atangaza kugombea tena jimbo kupia CCM


















Aliyekuwa mbunge wa wa Kinondoni kupitia CUF, kisha kujiuzulu na kuhamia CCM, Maulid Mtulia ametangaza nia ya kugombea tena ubunge jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)
-
Kupitia akaunti yake katika Mtandao wa kijamii, Mtulia amewaomba radhi wana Kinondoni kwa maumivu aliyowasababishia na kusema yupo tayari kuwaletea maendeleo kupitia CCM.


 "Kwaza, nawasalimu wote na khasa wananchi wenzangu wa jimbo la Kinondoni.

Pili, nawapa pole sana kwa maumivu makali mliyoyapata kutokana na uamuzi wangu wa kujiuzulu ubunge wa jimbo letu la Kinondoni kupitia chama cha CUF.

Tatu, nawahakikishia kwamba bado nawapenda sana na niko tayari kuwatumia tena kwa lengo la kuleta Maendeleo kwenye jimbo letu.
Hivyo basi, nichukie fursa hii kutangaza nia kwa wanakinondoni wote na watanzania kwa ujumla kuwa nitachukua form ya kuomba ridhaa kwenye chama changu cha CCM na endapo chama changu kitaridhia basi nitakuja mbele yenu kuomba ridhaa ya kuwatumikia katika nafasi ya ubunge wa jimbo letu Kinondoni.

Mimi mtumishi wenu,

#Maulid_Mtulia.

No comments:

Post a Comment