Baada ya madereva kutelekeza magari yao, ndipo wamilii wa magari hayo wakaamua kufanya jitihada za kutafuta madereva wengine ili kuwezesha abiria kuendelea na safari zao.
Hali hii ilisababisha abiria wengi kucheleweshewa safari zao na kusababisha malalamiko mengi. Hata hivyo wengi wa abiria wamelipongeza jeshi la polisi na kuwasihi operesheni hiyo iwe endelevu pamoja na kusimamia uzembe wa madereva ili kuepusha ajali za barabarani, hasa msimu huu wa sikukuu za christmas na mwaka mpya.
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha Bw. Joseph Charles amesema kuwa licha ya madereva hao kuwatoloka na kutokomea kusikojulikana, bado wataenelea kuwasaka na kuwachukuliahatua kali za sheria ili kukomesha tabia hii ya ulevi na uzembe kwa madereva.

No comments:
Post a Comment