Aliyekua Katibu mkuu wa chama kikuu cha Upinzani Tnzania, CHADEMA ateuliwa kuwa balozi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu, Dr Slaa ataapishwa karibuni baada ya taratibu kukamilika ikiwa ni pamoja na kupangiwa kituo chake cha kazi ambacho mpaka sasa hakijawekwa wazi
Kama inavyofahamika, Slaa alikua mwanasiasa machachari na aliyetumikia siasa kwa takribani miongo miwili kabla ya kuikacha CHADEMA mwaka 2015 baada ya ujio wa waziri mkuu wa zamani Mh, Edward Lowasa katika UKAWA na CHADEMA na kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Urais.
No comments:
Post a Comment