Watu 7 wamekufa na wengine kiasi cha 12 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la Saratoga
kugongana na Hiace katika kijiji cha Kabeba Mkoani Kigoma. Kamanda wa polisi mkoani humo Sweetbert Njewike
amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kusema kwmba chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa madereva wote wawili na kutokua makini barabarani.
"Eneo ilipotokea ajali ni eneo jembamba la daraja ambapo ni gari moja tu linapita kwa wakati mmoja, kwahiyo chanzo kikuu ni madereva hao kutokua makini " Amesema Njewike
Ameongeza kuwa hali za majeruhi zinaendelea vizuri na wanapatiwa matibabu katika kituo cha afya cha ilagala na waliopoteza maisha bado hawaja tambuliwa na wanafanya juhudi kupata majina yao na watatoa taarifa
#ITV Tanzania
No comments:
Post a Comment