Saturday, December 30, 2017
KUZUIA KUTAPIKA SAFARINI
Kitendo cha kutapika kinaweza kumtokea mtu yoyote na hii huchangiwa na
hali ya hewa inapoingiliana na utokea kwa wasafiri wa majini na nchi kavu, pia hutokea mara nyingi kwa mtu ambaye hakuwahi au hajawahi kusafiri umbali mrefu.
Ili uweze kuzuia hali hii uwapo sfarini basi huna budi kuepuka kula ovyo kabla ya kuanza safari na ndani ya safari, pia usile kula vitu vyenye sukari nyingi kwani vinaweza kuharibu koo lako kutoka na sukari kuzidi.
Vile vile unashauriwa kuweka njiti ya kiberiti mdomoni ili kuzuia kutapika, na kama hitoshi lamba ndimu kila wakati kwani inakata kichefuchefu na kutapika haraka.
Hivyo vyote vikashindikana na ukaona unahitaji kutapika basi muite muhudumu wa usafiri huo, ili akupatie mfuko wa rambo uweze kutapikie humo na ukimaliza hakikisha unafunga vizuri na kuweka sehemu husika na baada ya hapo safisha kinywa chako kwa maji safi na salama.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment