Ni kawaida sana kuona makundi mengi ya Wasap yakiundwa kwa madhumuni mbali mbali kote Nchini.
Kundi la Whatsap lijulikanalokama
'Wilaya Ya Ludewa' limekabidhi kitanda maalumu cha kubebea wagonjwa waliozidiwa kwa Hospitali ya Wilaya ya Ludewa chenye thamani ya takribani Tsh Milioni 1.4
|
Viongozi wa Kundi la Wasap la Ludewa District katika picha ya pamoja wakati wa kukabidhi kitanda na wahudumu wa Afya na Viongozi
|
Orodha ya Majina ya Washiriki (Members) wa Kundi hilo
Hili limekua ni jambo la kutakiwa kuigwa na makundi mbalimbali ya wasap nchini ili yasibaki kutumika tu ku chat mambo yasiyofaa au kuwa na manufaa, bali kuwa na tija na pia kusaidia Jamii.
Kiongozi wa Kundi la Wasap la Ludewa District Bw. Benjamin Mtweve
Kiongozi wa Kundi Hilo Bw. Benjamin Mtweve amesema "Kundi letu hili limekuwa likifanya hivi kila mwisho wa mwaka. Mimi kama Admn mkuu,nawashukuru sana wote waliofanikisha zoezi hili.
Toa Maoni Yako!!
|
|
No comments:
Post a Comment