SUBSCRIBE TO OUR YOUTUBE CHANNEL-Shec Media.........LIKE OUR FACEBOOK PAGE-Shec Media..... FOLLOW US ON INSTAGRAM-@shecmedia_tz........WHATSAPP NUMBER +255 752 0133 43

Thursday, January 18, 2018

Treni inayobweka kama mbwa kuwafukuza swara kwenye reli

Treni zingine huunda kuwa na sura ya mbwa
Treni iliyoundwa mfano wa Mbwa ili kuwatisha swala wanaolamba chuma cha reli usiku
Watafiti nchini Japana wameiwekea treni kipasa sauti ambacho kinabweka kama mbwa na kutoa mlio wa swara ili kuzuia treni kugonga swara njiani.

Gazeti la
Asahi Shimbun lilisema kuwa sauti hizo zinatumiwa kuwafukuza swara kutoka kwa reli kwa lengo la kupunguza idadi ya wanaogongwa na kuuawa na treni.

Swala ni wanyama waporini ambao hupenda sana kuramba chuma cha reli ili kujipatia madini muhimu mwilini mwao
Maafisa kutoka kwa taasisi ya reli wanasema kuwa mlio wa sekunde tatu wa swara humfanya swara kuwa makini na kusikiliza, ukifuatiwa na sekunde 20 za mbweko wa mbwa, inaweza kusababisha swara kukimbia.

Image result for train at night

Swara hukaribia reli nyakati za usiku kulamba chuma za reli wakitafuta virutubishi muhimu vya madini ya mwili.
Wizara ya uchukuzi nchini Japan inasema kuwa kulikuwa na visa 613 vya treni kugonga swara na wanyama wengine mwaka 2016.

TOA MAONI YAKO

No comments:

Post a Comment