Saturday, December 30, 2017
HAMFREY POLEPOLE: HAKUNA KIONGOZI WA DINI AMETISHWA KWA KUSEMA UKWELI
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole amewazungumzia Askofu Zakaria Kakobe pamoja na
baadhi ya viongozi wengine wa dini na kusema kuwa
hakuna mtu ambaye amezuiliwa kuongea Tanzania na kuwa wapo huru kutoa maoni yao.
Polepole alisema hayo juzi wakati akihojiwa na kituo kimoja cha Television na kusema hakuna mtu ambaye ametishwa kwa kusema ukweli juu ya jambo fulani ambalo huenda lipo au linatokea Tanzania.
"Hakuna mtu amezuiliwa kuongea ukweli ndani ya nchi ya Tanzania, hakuna mtu ametishwa kwa kusema ukweli na hasa katika uongozi wa awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, anayesema mtu Tanzania kuna mtu kazuiliwa kuzungumza uhuru wake wa maoni nadhani atakuwa na matatizo ila nachofahamu kwamba mtu kuzungumza lugha ya matusi kwa mujibu wa Katiba yetu na sheria zetu ni makosa" alisema Polepole
Polepole aliendelea kusisitiza kuwa viongozi hao wa dini wapo wazi na huru kusema chochote kile kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
"Wapo huru kusema chochote kwa mujibu wa Katiba yetu ya nchi na sheria za nchi na nitasema neno moja dogo kitu ambacho na mimi ninatoa rai, nitakapokaa vizuri nitafafanua vizuri mambo haya lakini ukiwa kiongozi yoyote yule kauli ni jambo la msingi sababu una watu wanakufuata" alisisitiza Polepole
Juzi Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Mst. Projest Rwegasira, ilitoa onyo na kuwataka viongozi wa jumuiya za kidini kutotumia mahubiri yao ya ibada kwa kufanya uchambuzi wa masuala ya siasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment