SUBSCRIBE TO OUR YOUTUBE CHANNEL-Shec Media.........LIKE OUR FACEBOOK PAGE-Shec Media..... FOLLOW US ON INSTAGRAM-@shecmedia_tz........WHATSAPP NUMBER +255 752 0133 43

Friday, December 1, 2017

TFF YAMJIBU ZITTO KABWE






















Shirikisho la Soka Tanzania TFF limejibu hoja iliyotolewa na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, kuitaka Tanzania isusie kucheza mechi na Libya ili kupinga vitendo vya biashara ya utumwa inayoendelea nchini humo.


Akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio, afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema suala hilo limefikishwa kwa uongozi wa TFF na litatolewa majibu hivi karibuni.
"Msimamo utatolewa na viongozi wangu mara baada ya kukaa na kutafakari hali halisi kwa sasa, na wenye uwezo wa kukaa na kutafakari ni viongozi wa juu, itakapokuwa tayari mtajulishwa", amesema Alfred Lucas.
Hapo jana Zitto Kabwe ametoa wito kwa TFF kuitaka timu ya Kilinajaro Stars isusie mechi inayotarajiwa kuchezwa na Libya, ili kuonyesha kutokubaliana na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kuendeleza biasha ra utumwa.

#Source: #EATV

No comments:

Post a Comment