Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametangaza baraza jipya la mawaziri huku akiwateuwa maafisa waandamizi wa jeshi hilo katika bara hilo
Rais Mnangagwa amemteuwa Generali Sibusiso Moyo, ambaye ndiye aliyetangaza mapinduzi katika Television ya taifa kuwa Waziri mpya wa Mambo ya Nchi za Nje,Wakati Kamanda wa Kikosi cha Anga Perence Shiri, ameteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo na Masuala ya Ardhi.
Katika uteuzi huo Rais pia amemteuwa aliyekuwa Kiongozi wa Chama cha Wapiganaji wa zamani wa vita Chris Mutsvangwa, kuwa Waziri wa Habari.
Taarifa hiyo inasema Rais Mnangagwa amewabakiza mawaziri wengi waliokuwa katika utawala wa Rais Mugabe, uteuzi ambao kiongozi wa chama cha upinzani Tendai Biti ameuponda uteuzi huo kwa kusema kwamba matarajio ya wazimbabwe hayakuwa sahihi ya kutarajia mabadiliko.

No comments:
Post a Comment